Nyota wa muziki wa bongo flava na mtunzi wa mashairi kutoka jumba la vipaji la THT, Elias Barnabas ‘Barnaba’ anatarajia kuanza kushoot video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha Mr. Blue mapema wiki ijayo.
Akiongea na Hivisasa blog Barnaba alisema kuwa video ya wimbo ‘Marry You’ alioutunga maalumu kwa ajili ya mama watoto wake na wale wote wenye mapenzi ya dhati kwa wenzi wao utaanza kutengenezewa video yake hivi karibuni kwani mapema wiki ijayo ataingia location na Mr. Blue kwa ajili ya kuandaa video hiyo.
Barnaba aliongeza kuwa alifanya wimbo huo na Mr. Blue kwa sababu alifaa kuwa katika nafasi hiyo kutokana na jinsi anavyomkubali katika kazi zake hivyo video hiyo itakuwa kali kama ulivyo wimbo japo hakusema nani ataongoza video hiyo.
Katika hatua nyingine Barnaba anayeishi na familia yake kwa sasa anategemea kufunga ndoa na mama watoto wake hivi karibuni hivyo wimbo ‘Marry You’ umetoka katika wakati muafaka hasa katika maisha yake.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment