Ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Lumumba jijini Dar es salaam imebomolewa kwa kutumia tinga tinga ili kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye amesema kuwa jengo hilo limebomolewa kwa lengo la matengenezo ya kawaida.
Ameongeza kuwa viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho watatumia jengo la Umoja wa Vijana chama cha Mapinduzi lilipo barabara ya Morogoro.
Katika hatua nyingine baadhi ya makada waliokataa kutaja majina yao walisema kwamba jengo hilo limebomolewa kupisha ujenzi wa jengo la kisasa kwa ajili ya kitega uchumi ambapo chama kitajipatia mapato kutokana na jengo hilo
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment