WENYEVITI WAPYA WA SERIKALI ZA MITAA WATAKA WALIPWE MISHAHARA

WENYEVITI wa serikali za mitaa na wajumbe wao katika Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji wameapishwa jana kuanza kutumikia wananchi kulingana na nafasi zao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, walitaka serikali kuangalia suala la kulipa mishahara kila mwezi kwa wenyeviti na wajumbe hao. Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnazi Mmoja, kata ya Kitongoni Manispaa ya Kigoma Ujiji, Nuru Bashange alisema nafasi ya wenyeviti wa mitaa na wajumbe wao itambulike rasmi kikatiba na walipwe mishahara kama wanavyolipwa wabunge na madiwani. Bashange alisema wenyeviti wa maitaa na wajumbe wao wamekuwa na jukumu kubwa la kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Alisema imefika wakati sasa wa serikali wa kuona umuhimu wa kuwapatia mafao ya kutosha kila mwezi viongozi hao badala ya posho ya Sh elfu kumi kwa mwezi inayolipwa sasa. Mwenyekiti huyo wa Mtaa alisema hata kama madiwani hawalipwi mishahara lakini kiwango cha posho wanacholipwa hakina uwiano na kiwango wanacholipwa wenyeviti wa mitaa. Kwa mujibu wake, ni wakati wa kufanya maboresho kwenye malipo kuwatia moyo wenyeviti hao katika kusimamia utendaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo bila kufuata vishawishi. Pamoja na madai hayo kwa serikali wenyeviti hao wameahidi kutumia nafasi zao katika kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo kama ambavyo nia na dhamira yao iliwatumia na kuamua kugombea nafasi hizo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: