KITUKO:.....MAMA AMFUKUZA NYUMBANI MTOTO WAKE WA MIAKA 12 NA KUMTAKA AKAPANGE BAADA YA KUUNGUZA MBOGA JIKONI

Mtoto wa miaka 12 mkazi wa Mkoa wa Geita ametimuliwa nyumbani na mama yake mzazi na kutakiwa kwenda kuishi maisha ya kujitegemea baada ya kuunguza mboga jikoni. Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Karangalala ameamuriwa na mama yake kufanya hivyo baada ya mama yake Helena kumwachia jukumu la kupika mboga Novemba mwaka jana lakini mboga hiyo iliungua. Baada ya kuunguza mboga hiyo,mama huyo alimpiga mwanaye kabla ya kumpa masurufia na kumkabidhi chumba tayari kwa kuanza maisha. Mtoto huyo alisema mama yake amekua na tabia ya kumpiga mara kwa mara kiasi cha kusababisha mwili wake kuwa na alama za viboko. “Sifahamu kwa nini mama yangu huwa ananipiga kiasi hiki,inawezekana kwa kuwa na yeye alilelewa na mama wa kambo aliyekua anampiga hivi”alisema mtoto huyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: