Hofu imetanda kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya na Mikoa ya jirani baada ya kuzagaa kwa samaki wanaodaiwa kufa kwa sumu iliyotoka kwenye migodi ya nchi ya jirani yaMalawikutokana na maji yake kutiririka kuelekeaZiwa Nyassa.
Taarifa za kuingizwa kwa samaki hao wanaodaiwa kuwa walikufa kwa sumu kwenye masoko mbalimbali Wilayani Kyela, Rungwe na Mbeya zilitolewa jana kwa mtandao na baadaye kutolewa tamko na viongozi wa Serikali.
Samaki hao wanadaiwa kuanza kufa tangu Januari 10 nchini Malawi na kwa upande wa Tanzania wameonekana tangu Januari 11 na kwamba hivi sasa wapo wanaoelekea majini kana kwamba wameanikwa.
Taarifa hiyo ilizua hamaki miongoni mwa wakazi ambapo Msaidizi mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoroaliyetajwa kwa jina la Marco Masaya alipoulizwa kama wanayo taarifa ya kuzagaa kwa samaki hao alijibu kuwa ni kweli.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment