Miili ya waliofukiwa kifusi mgodini yaopolewa

Hatimaye wachimbaji wote watatu waliokufa kwa kufukiwa na kifusi cha jabali katika mgodi wa dhahabu wa Onesmo Goldmine Mawemeru uliopo katika kijiji cha Nyalugusu Wilayani Geita imeopolewa jana usiku baada ya juhudi za siku nne.
Hatua hiyo imedaiwa ni matokeo ya ushirikiano na mshikamano mkubwa uliooneshwa katika kutekeleza zoezi hilo kati ya Uongozi wa Mgodi huo, wadau na serikali ya wilaya na mkoa zoezi lililokuwa linafanyika usiku na mchana kwa kushirikisha wadau tofauti na hivyo kufanikiwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Joseph Konyo akithibitisha LEO kupatikana kwa miili hiyo alisema kazi hiyo ilihitaji ujasiri na kujituma na ndicho kilichofanyika kuhakikisha miili yote mitatu imeopolewa.
Amewataja miili yao walioopolewa kuwa ni Benjamin Yusuph, Robert Edward na Nsulwa Bungila ambao wote walifukiwa katika mgodi huo Januari 11 saa moja usiku na wengine wanne Samson Haroun, Rutu William, Faida Bukombe na Seif Ally waliokolewa siku ya tukio.
Akizungumzia hatua hiyo jana Mkurugenzi wa Mgodi huo Malugu Onesimo Gelewa alisema toka usiku tukio la ajali lilipotokea wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana ya kuitafuta miili hiyo chini ya mafundi na wadau wengine na hatimaye kufanikiwa.
''Miili yote mitatu imepatikana usiku wa kuamkia leo Januari 15, kwa nyakati tofauti na mwili wa mwisho ambao ni watatu umepatikana alfajiri ya kuamkia jana na tayari imesafarishwa kwa ajili ya maziko makwao.
Awali akitoa salaam za rambirambi za serikali kwenye eneo la tukio mkuu wa mkoa wa Geita Fatma Mwasa Juzi aliwaomba wananchi wakiwemo waliofikwa na msiba huo kuwa wavumilivu kutokana na ajali hiyo na kusisitiza watu wote ikiwemo serikali ilikuwa imeguswa na msiba huo na kutaka tahadhari zaidi kuchukuliwa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: