Escrow yamng’oa madarakani Prof. Muhongo

Sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow limechukua sura mpya kufuatia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kutangaza kujiuzulu mbele ya Waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dares salaam Hatua hiyo inafuatia Maazimio ya Bunge yaliyotaka Waziri wa Nishati na Madini awajibishwe kutokana na kutowajibika suala lililopelekea upotevu wa mabilioni ya fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow. Aidha, maazimio ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali chini ya Bw. Zitto Kabwe ilitokana na sakata la ufisadi wa Akaunti ya Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 306 zilichukuliwa kiholea Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha mjadala mzito ndani na nje ya Bunge. Katika sakata hilo mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na uchuguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwenye akaunti hiyo ulibainisha kuwa katika fedha zilizochotwa Benki kuu ndani yake kuna kodi umma iliyoibwa. Kwa mujibu wa uchunguzi wa Takukuru ulibainisha kuwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, Waziri wa Madini na Nishati, Profesa Sospiter Muhongo pamoja na watendaji wengine serikalini wamehusika katika upotevu wa fedha hizo katika akaunti ya Tegeta Escrow ama kwa kukusudia ama kwa kutojua, kitu ambacho kilielezwa kuwa ni uzembe. Kufutia suala hilo Rais Jakaya Kikwete alichukua uamuzi wa kumuondoa madarakani Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kutokana na madai kuwa alipewa shilingi Bilioni 1.6 zilizotoka katika akaunti hiyo ya Escrow suala ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma. Katika mkutano wake na wazee jijini Dares salaa Rais Kikwete alisema Profesa Muhongo alikuwa amemuweka kiporo,hadi leo ambapo prof. Muhongo ametangaza kujiuzulu rasmi nafasi hiyo
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: