MKOA WA MBEYA WAIOMBA IDARA YA MAMBO YA KALE KUWAKABIDHI MAKUMBUSHO YA MAMBO YA KALE YA KIMONDO

MKOA wa mbeya umepania kuboresha miundo ya kituo cha mambo ya kale cha Kimondo wilayani Mbozi mkoani hapa iwapoIdara yaMambo ya kaleiliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii itakubali ombi la mkoa huo kukabidhi kivutio Halmashauri ya Mbozi. Hatua hiyo imekuja kufuatilia ziara ya wanahabari mkoani Iringa wanaotembelea vivutio vya utalii mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa kama njia ya kuhamasisha utalii mkoa ya nyanda za juu kusini na pia kubaini sababu za utalii kutokua kwa kasi katika mikoa hiyo. Mhifadhi msaidizi wa kituo cha makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo wilayani Mbozi Bw Mussa Nsojo alisema kuwa mbali ya watalii wengi kupenda kutembelea eneo hilo la Kimondo ila miundo mbinu ya eneo hilo si rafiki kwa watalii kuendelea kutembelea kutokana na serikali kushindwa kuboresha majengo na eneo hilo kwa ujumla. Alisema kuwa kimondo hicho ambacho mwaka kilipoanguka eneo hilo haufahamiki ila utafiti wake ulianza kati ya mwaka 1930 -1931 na kubainika kuwa si jiwe la kawaida bali ni sayari iliyoanguka kutoka angani toka wakati huo kimendelea kupata umaarufu wa watalii kufika kutembelea eneo hilo japo katika eneo hilo mazingira yake ni mabovu zaidi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: