Klabu ya Real Madrid ya Hispania imevunja rekodi kwa kuwa timu tajiri zaidi duniani kwa miaka 10 mfululizo, kampuni ya Delloite imedhibitisha. Utajiri kwa Real Madrid unatokana na matangazo,mauzo ya jezi kutokana na kuwa na wachezaji ghali zaidi Duniani kama Ronaldo,Bale na James Rodriguez huku moja ya chanzo kingine kikubwa kinachofanya klabu kuingiza pesa ni mapato kutokana na uwanja wake wenye uwezo wa kuingiza watazamaji zaidi ya 80.000.
Kwenye orodha hiyo Real Madrid inafuatiwa na Manchester United kwenye nafasi ya pili na Bayern Munich na Barcelona zikifuatia.
Real Madrid imepata mapato makubwa kutokana na kuchukua klabu bingwa barani Ulaya kwa kuifunga Athletico kwa magoli 4-1 huku klabu zote 20 zikiongezeka kimapato kutokana na matangazo ya televisheni kutoka asilimia 8 na 9.
Orodha ya vilabu 10 tajiri zaidi Duniani
1. Real Madrid: 549.5m (518.9m)
2. Man Utd: 518m (423.8m)
3. Bayern Munich: 487.5m (431.2m)
4. Barcelona: 484.6m (482.6m)
5. Paris Saint Germain; 474.2m (398.8m)
6. Manchester City: 414.4m (316.2m)
7. Chelsea: 387.9m (303.4m)
8. Arsenal: 359.3m (284.3)
9. Liverpool: 305.9m (240.6m)
10. Juventus: 279.4m (272.4m)
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment