DC apiga Marufuku Matumizi ya Maji kuhofia Afya za Wanakijiji

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Benson Mpesye Kutokana na kuvuja kwa bwawa la maji la Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Bulyankulu yanayosadikika kuwa yana sumu ya Syned Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Benson Mpesye amepiga marufuku wananchi wa kijiji namba 9 katika kata hiyo kutumia maji ya kisima pamoja na kuendesha shughuli za kilimo. Mpesye amesema kuwa serikali imeamua kupiga marufuku utumiaji wa maji pamoja na shughuli za kilimo katika kijiji hicho mpaka hapo Balaza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) litakapomaliza uchunguzi wa kemikali hizo. Aidha ameyataja madhara yaliyotokea kutokana na maji hayo ni kukauka kwa mazao na maji kubadilika rangi tofauti na yaliyokuwa awali pamoja jambo linaloweza kupelekea magonjwa endapo wataendelea kutumia maji hayo. Kwa upande wake Ofisa Usalama wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyankulu Abdallah Mssika amesema kuwa kufuatia tukio hilo uongozi umeimarisha miundombinu ya visima na kuahidi kuwa hali hiyo aitaweza kujirudia.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: