Msanii wa filamu za Kibongo, ‘Yusuf Mlela’ amefunguka kuwa baada ya kuishi ‘singo’ kwa muda mrefu, sasa ameamu kujipanga kuoa hivyo ndani ya mwaka huu lazima ndoto yake hiyo itimie.
Mlela alisema mwaka huu amejiwekea malengo mengi lakini kubwa zaidi ni kuoa kwani anahisi akiendelea kuwa peke yake kuna mambo atakwama kwa kuwa hatakuwa na mtu wa kumshauri kwa karibu.
“Kiukweli maisha yenyewe ni mafupi na umri nao unaenda hivyo lengo langu kubwa kwa mwaka huu ni kuoa na kuhusu nitamuoa nani, itajulikana baadaye lakini kwa sasa tambueni kwamba mwaka huu lazima nioe, nimechoka maisha ya ubachela,” alisema Mlela.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment