Rais wa Ghana, John Mahama, amesema kwamba msaada wa kimataifa unahitajika kuweza kulishinda kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, nchini Nigeria.
Aidha, Rais Mahama alisema nchi moja pekee haiwezi kuwashinda wapiganaji hao na kwamba ugaidi kila pahala ni tishio la dunia nzima.
Ameongeza kuwa viongozi wa nchi za Afrika Magharibi watakutana juma lijalo kuomba idhini ya Umoja wa Afrika kuunda kikosi cha kimataifa ili kupambana na Boko Haram, lakini aliongeza kusema kuwa kutuma kikosi hicho kunaweza kuchukua miezi.
Kwa upande mwingine wanajeshi wa Chad wameanza kujongea Cameroon, kama sehemu ya ushirikiano zaidi wa kanda hiyo ili kuisaidia nchi ya Nigeria kupambana na wanamgambo wa Boko Haram.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment