Makanisa yachomwa Niger kisa Gazeti la Charlie Hebdo

Makanisa matatu yamechomwa nchini Niger katika mji wa Niamey ikiwa ni siku ya pili ya maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa na gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange. Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwao
Polisi wa kukabiliana na ghasia kwa sasa wameweka ulinzi mkali katika kanisa la Cathedral mjini humo ambapo makundi ya vijana wanarushia mawe.
Siku ya ijumaa watu wanne walifariki huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya waandamanaji kuyapekua makanisa matatu kabla ya kuyachoma mbali na kukichoma kituo kimoja kilicho na utamaduni wa Ufaransa huko Zinder.
@
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: