umechishaji kwa upande wa nguo za vitenge na mikoba pamoja na mabegi.
Kumechisha ni aina ya uvaazi uliopo kwenye fasheni wakati huu ambapo mvulana au msichana anavaa mavazi yanayofanana rangi. kwa mfano shati rangi ya bluu na kiatu rangi ya bluu au kuvaa nguo zenye rangi zinazoendana.
Ingawa kumechisha kupo kwenye chati katika suala zima la urembo, mitindo na mavazi, lakini hilo halizuii ladha ya rangi mchanganyiko.
Kwa baadhi ya watu kumechisha, kumekuwa ni kama kanuni, ili kujiweka maridadi zaidi, ila kwenye mitindo, unaweza kuwaza zaidi katika hilo. Mtindo wa mavazi ya rangi rangi ukipangiliwa vizuri mwilini ni dhahiri huvutia.
Wabunifu wa mavazi wamejaribu kuzitumia rangi mbalimbali vizuri na kumfanya mvaaji
kuonekana kama ua machoni mwa watu. Unaweza kuchanganya rangi hizi kuanzia katika viatu, mavazi, vipuri, mkoba na hata ya rangi ya nywele, kwa kadri utakavyoona inafaa, na isikupe shida sana.
Muhimu ni kuzingatia kwamba, rangi utakazochanganya kwanza zinaendana, katika mpangilio wa rangi, na pia zinaendana na rangi ya mwili wako.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment