PHIRI AKUMBUSHIA ALIVYOACHA KAZI NAMIBIA KUIFUATA SIMBA

i wish you happy chrismass and happy new year




Kocha Patrick Phiri ambaye amefutwa kazi Simba amekumbushia jinsi alivyoacha kazi ya ukocha wa timu ya taifa ya Namibia kuja Simba.


Alisema alipata ofa nzuri kutoka kwa Shirikisho la Soka Namibia ambapo alikuwa aende kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, lakini akaamua kuja Simba kutokana na heshima aliyowapa.

Phiri ambaye alitarajia kuondoka jana amefungishiwa virago kwa kile kilichosemwa kuwa ni kutokana na mwenendo mbovu wa timu ambapo amefungwa mechi moja tu kati ya nane dhidi ya Kagera Sugar wiki iliyopita.

Phiri amesema kuwa kabla ya Simba kumhitaji alikuwa na ofa nzuri nchini Namibia, lakini aliamua kuja Simba kutokana na kuifahamu vema hivyo isingekuwa kazi ngumu kwake pia na mapenzi makubwa aliyonayo kwani ameifundisha mara kadhaa.

“Nilikuwa na ofa kule Namibia tena nzuri, lakini niliamua kuwasikiliza Simba kwa kuwa kwanza ni timu yangu, nimekuwa nao kwa muda mrefu, pia nilijua ingekuwa kazi rahisi kwangu kwa kuwa si mazingira mageni kwangu.

“Siwezi kusema kuwa Simba ilikuwa imenishinda ila wenye maamuzi ni wao (viongozi) wanaojua wapi penye udhaifu katika timu yao. Nadhani hii ni mara yangu ya tatu kuja Simba kwa hiyo nilijua mambo yangekuwa rahisi kwangu kutokana na kuifahamu vema,” alisema Mzambia huyo ambaye alikuwa akikunja kitita cha milioni nane kwa mwezi.


Nafasi yake imechukuliwa na Mserbia, Goran Kopunovic ambaye kibarua chake cha kwanza kitakuwa kwenye Michuano ya Kombe la Mapinduzi huku Visiwani Zanzibar.
  • @salehe jembe
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: