i wish you happy chrismass and happy new year
Ili kuhakikisha inawashambulia zaidi wapinzani kila mara, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm, amewapiga marufuku viungo wake Haruna Niyonzima na Salum Telela kurudisha mipira nyuma wakiwa wanaelekea goli la wapinzani wao.
Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni jijini Dar kabla ya kuelekea Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi, linaloendelea visiwani humo.
Pluijm amesema kuwa viungo wake hao ndiyo waliocheza bila kufuata maelekezo yake ambayo ni kucheza soka la pasi za haraka na kupiga pasi za nyuma wakati wanalishambulia goli la wapinzani wao.
Pluijm alisema hilo ameliona na mengine likiwemo suala la mawasiliano kati ya mabeki na kipa wake jambo lililosababisha bao la pili la John Bocco.
Aliongeza kuwa, amepanga kuufanyia kazi upungufu aliouona kwenye mechi za Kombe la Mapinduzi na katika mazoezi yake huku akiendelea kuwapa mbinu wachezaji katika kukijenga kikosi chake.
“Kabla ya mechi ya Azam FC, niliwakataza viungo wangu kucheza pasi za nyuma wakati tukiwa na mpira, badala yake kulishambulia goli la wapinzani wetu kwa kasi, lakini wenyewe walicheza pasi nyingi za nyuma kitu ambacho sijawaelekeza, hali hiyo iliwapa Azam FC nafasi ya kupumzika,” alisema Pluijm.
0 comments:
Post a Comment