i wish you happy chrismass and happy new year
Kocha Msaidizi ya Simba, Selemani Matola, juzi usiku alijikuta akidondosha machozi baada ya timu hiyo kuchezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani hapa.
Kutokana na hali hiyo, Matola aliwashushia lawama wachezaji wa kimataifa timu hiyo kutoka Uganda ambao hawakuambatana na kikosi hicho visiwani hapa kwa ajili kushiriki Mashindano ya Mapinduzi yalioanza juzi Alhamisi.
Waganda hao ni Emmanuel Okwi, Simon Sserunkuma, Juuko Mrushid na Joseph Owino ambao kwa pamoja hawakuweza kuambatana na kikosi hicho kutokana wote kudaiwa kuwa kwao nchini Uganda.
Matola amesema kuwa kikosi chake kimeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo kutokana na kukosekana kwa nyota hao.
“Kukosekana kwa wachezaji wa kimataifa ndiyo hasa kumesababisha tupate matokeo haya kwa sababu nimelazimika kuchezesha wachezaji wasiokuwa na uzoefu wa mashindano, hivyo nadhani jambo hili viongozi watakuwa wameliona na watalifanyia kazi,” alisema Matola.
0 comments:
Post a Comment