PAC yamtaka Wassira kuhama nyumba ya Bodi ya Sukari

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira ameatakiwa kuhama katika nyumba ya Bodi ya Sukari Tanzania kufuatia kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kutoa amri hiyo kutokana na kuishi katika nyumba hiyo kinyume na taratibu
Aidha, Wasira akiwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika alikuwa akiishi katika nyumba hiyo inayomilikiwa na SBT iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SBT, Henry Semwaza aliieleza Kamati ya PAC jana katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, kuwa wamekuwa wakifanya jitihada za kuwasiliana na Wasira kuhusu kuirejesha nyumba hiyo, lakini hakuna utekelezaji wowote unaofanyika.
Kufuatia Wassira kutotekeleza wito wa kuhama Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akitoa azimio la Kamati hiyo alisema, “Hapa hakuna msukumo mnaoufanya yaani tangu mwaka 2012 mlipomwandikia barua mpaka sasa kimya. Tunaiagiza SBT kumwandikia barua Wasira mkimtaka arejeshe nyumba na nakala ya barua hiyo tuipate Jumatatu (Januari 19 mwaka huu).”
Ameongeza kuwa kutokana na kuwapo kwa harakati za kutaka kubadili hati ya umiliki ya nyumba hiyo, Zitto alisema, “Msajili wa Hazina kamati inakuagiza uhakikishe umiliki wa nyumba hiyo unabaki kwa bodi ya sukari na si vinginevyo.”
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa PAC Zitto pia alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Sophia Kaduma amwandikie barua Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu uamuzi huo wa Kamati.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: