SOW AIFUNGIA SENEGAL BAO LA USHINDI JIONI, GHANA YALALA 2-1

Moussa Sow aliyeingia kipindi cha pili ameifungia Senegal bao la pili katika dakika za majeruhi na kuiwezesha kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ghana.
Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa timu hizo hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika inayofanyika nchini Equatorial Guinea.
Ushindi huo ni muhimu kwa Senegal ambayo ipo kundi C maarufu kama kundi la kifo kwa kuwa timu nyingine ni Algeria na Afrika Kusini.
Ghana ilitangulia kupata bao kwa mkwaju wa penalti kupitia Andre Ayew. Lakini Senegal wakasawazisha.
Kipindi cha pili kilikuwa na ushindani mkubwa na Simba hao wa Milima ya Terranga walifanikiwa kupata bao zikiwa zimebaki sekunde kumi kabla ya mpira kwisha baada ya dakika tatu kuwa zimeongezwa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: