Meneja wa msanii wa Wema Sepetu, Martin Kadinda, amekanusha taarifa za Wema, kumpeleka mahakamani aliyekuwa mpenzi wake Naseeb Abdul “Diamond”, kwa kile kilichosemwa ni kumtapeli shilingi milioni 10.
Kadinda, amesema kutokana na taarifa zilizoandikwa katika magazeti fulani nchini kuwa wanadaiana milioni kumi, sio kweli na kuongeza kuwa wawili hao hawadaiani kitu chochote na kuwa tuhuma hizo sio za kweli.
Amesema kuwa anashangaa taarifa hizi zimetoka wapi na kusema kuwa wanatafuta waanzilishi wa habari hizo ambazo hazina ukweli wowote na kuongeza kuwa anashangaa kuona habari hizo zimeandikwa bila ya yeye wala wahusika kuhusishwa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment