LEBANON YAANZISHA SHERIA MPYA KWA WASYRIA

Lebanon na Syria ni nchi zilizo karibu na wananchi wote huingia bure bila vikwazo baina ya nchi hizo,Lebanon yaanzisha matumizi ya Visa kwa Wasyria wote wanaoingia nchini Lebanon kwa mahitaji yafuatayo,Utalii,matibabu na wamiliki majumba.Sheria ya matumizi ya Visa ni pigo kubwa hasa kwa Syria ambayo ina machafuko ambayo uchangia raia wake kuhama nchi yao na kwenda kupata hifadhi nchi nyingine ikiwemo Lebanon, na kwa raia ambao wanasajili Ubalozini kwa ajili ya Utalii inabidi kuonyesha kielelezo cha Hotel unayofikia na pia kuwa na kiasi cha Dola 1000 ndipo utaruhusiwa kuingia,Afisa mmoja ambaye akutaka jina lake kujulikana amesema lengo kubwa la kuanzisha Sheria hii ni Ulinzi,kiuchumi na kujua idadi ya wageni waliopo nchini kwao. Kabla ya hapo wananchi wa Syria walikuwa wanaweza kuishi nchini Lebanon kwa miezi 6 bila tatizo na baada ya hapo ndio wanaweza kujisajiri kihalali, idadi ya wananchi wa Syria ambao wanaishi halali ni milioni moja na wengine laki tano bila vibali.Licha ya gharama za maisha nchini Lebanon ni juu bado idadi kubwa ya wakimbizi ukimbilia nchini humo kukimbia mapigano na hivyo kuchangia kuishi watu 10 mpaka 15 kwenye chumba kimoja.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: