Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jijini Dares salaam imekanusha madai yaliyotolewa na kambi rasmi ya upinzani kuwa Rais Kikwete amelidharau Bunge kwa kumuacha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo kuteua wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Tanesco.
Aidha,viongozi hao wa kambi ya upinzani Bungeni ambao ni Freeman Mbowe (Chadema) pamoja na David Kafulila wa NCCR-Mageuzi wamedai kuwa Ikulu na Rais Kikwete kumruhusu Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo kuteua wajumbe wa wapya wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni dhahiri amewadhalilisha Wabunge kwa kuwafanya waonekani wajinga kutokana na maazimio yao kutupwa.
Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imefafanua kuwa Madai hayo ya Kambi ya Upinzani, ambapo imesema kuwa kamwe Rais hajapata kulidhalilisha Bunge amaWabunge bali amefurahishwa na kazi yao nzuri na ushirikiano wao kwa serikali yake.
Imeongeza kuwa hadhi ya sasa ya Prof Muhongo kama Waziri wa Nishati na Madini bado inampa madaraka ya uteuzi kwa bodi zilizoko chini ya Wizara yake na wala hajapoteza sifa kuendelea kuwa ofisini na hivyo kukosa sifa ya kuteua Wajumbe wa Wakurugenzi wa Tanesco kama wanavyodai wabunge hao.
Katika hatua nyingine Ikulu imesisitiza kuwa uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ni hatua nyingine isiyopingika kuwa ni utekelezaji wa maazimio ya Bunge. Hata hivyo imewataka viongozi hao wa kambi ya Upinzani wakubali kufuata misngi ya haki katika kuwashughulikia watu wengine.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment