i wish you happy chrismass and happy new year
Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Yanga Mganda, Hamisi Kiiza amefanikiwa kupata dili Uarabuni (Oman), katika timu ya Fanja FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
Mshambuliaji huyo aliachwa na klabu yake kipindi cha dirisha dogo na nafasi yake kuchukuliwa na straika Mliberia, Kpah Sean Sherman.
Kiiza ameichezea Yanga kwa mafanikio makubwa tangu msimu wa mwaka 2012 na msimu uliopita alifanya vema baada ya kuifungia mabao 12.
Kwa mujibu wa chanzo ambacho ni ndugu wa kiungo huyo mshambuliaji huyo kwa sasa yuko katika michakato ya kuelekea Uarabuni kwenda kusaini katika timu hiyo au nyingine ambayo haikuitaja.
“Kiiza tulikuwa wote hapa nchini, lakini kaondoka Jumatano ya wiki hii kurudi Uganda kisha atakwenda Uarabuni kwa ajili ya kucheza soka, hapa nchini alifuata barua yake Yanga hivyo sijajua kama amepewa au la,” alisema ndugu huyo.
0 comments:
Post a Comment