i wish you happy chrismass and happy new year
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm juzi usiku alitumia dakika 90 kuzisoma timu za Simba na Mtibwa Sugar zilipokuwa uwanjani zikiumana kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hata hivyo, kasi kubwa ya wachezaji wa Mtibwa katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, ilimtisha kocha huyo ambaye alifika uwanjani hapo akiwa na ‘diary’ aliyokuwa ‘akinoti’ matukio yaliyokuwa yakiendelea ndani ya uwanja.
Lakini pia mara kwa mara alikuwa akishauriana na msaidizi wake, Charles Mkwasa, ambaye anaijua vema Mtibwa Sugar ambayo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo, kwa sasa timu hiyo ndiyo tishio kubwa kwa Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu Bara.
“Mtibwa Sugar wamecheza vizuri, wameonyesha kuwa si timu ya kuidharau hivyo nimejifunza jambo kutoka kwao,” alisema Pluijm.
0 comments:
Post a Comment