i wish you happy chrismass and happy new year
Habari tulizozipata hivi punde katika chumba cha habari cha Malunde1 blog zinasema kuwa kumetokea vurugu za aina yake katika makaburi ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga wakati wa mazishi ya mwanamke mmoja aliyekuwa anaishi katika mtaa wa Mapinduzi Juma Matv kata ya Ndala aliyefariki dunia juzi wakati akiumwa tumbo.
Tukio hili limetokea mchana huu.
Habari zinasema kuwa ndugu wa mwanamke huyo anayetokea Musoma (Mkurya) walikuwa wanataka ndugu yao apasuliwe tumbo wafanye mambo ya kimila makaburini lakini uongozi wa eneo husika wakasema utaratibu huo ungefanyika hospitalini badala ya hadharani watu wakishuhudia.
Tunaambiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa ameolewa Shinyanga na alipofariki mwili wake ulihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Mgogoro huo ulianzia nyumbani kabla ya kwenda makaburini,ndugu walitulia na wakati mazishi yanaendelea ndipo ndugu wa marehemu wakaingia kaburini kuzuia wananzengo wasitupie udongo makaburini.
"Mchungaji alipomaliza ibada ya mazishi akaruhusu mwili uzikwe,wananzengo wakaanza kutupia udongo,ghafla ndugu wa marehemu wakaingia kaburini na kuzuia wananzengo,wakatoa mwili wakauchana kwa wembe,wakachinja kuku,wakamwagia damu mwili wa marehemu na kumwingiza kwenye tumbo la marehemu huyo kuku,kisha wakaaanza kuzika upya",mmoja wa mashuhuda ameiambia malunde1 blog.
"Kitendo cha ndugu kung'ang'ania kufanya mambo yao,kiliwakera wananchi wakaamua kutoka makaburini,na jeshi la polisi limefika eneo la tukio na kuwakamata ndugu wote wa marehemu",aliongeza shuhuda huyo.
Na Kadama Malunde-Shinyanga

0 comments:
Post a Comment