JAVU AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUJERUHIWA ‘TAYA’ ZANZIBAR

MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Hussein Javu alikimbizwa hospitali mwishoni mwa mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa ya Jang’ombe baada ya kuumia. Javu alitokea benchi dakika ya 65 kwenda kuchukua nafasi ya Mbrazil, Andrey Coutinho lakini baada ya dakika 20 akaumia na kutibiwa kwa dakika mbili kabla ya kupakizwa kwenye gari kukimbizwa hospitali. Javu alipigwa daluga la sehemu ya mdomoni (taya) na mchezaji wa Taifa na kuumia, hivyo nafasi yake akaingia Rajab Zahir dakika ya 86 kumalizia mchezo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: