MUHONGO ATEUA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI TANESCO

Waziri wa Nishati na madini Prof Sospeter Muhongo amewateua wajumbe wapya wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Aidha wakurugenzi wa Bodi hiyo wataongozwa na Dk Mighanda Manyahi ambaye ameteuliwa na Rais Jakaya kikwete. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo ambayo imesainiwa na Kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo, imesema kuwa Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo amewateua wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo ambao wameshaanza kazi hivi sasa. Kwa upande wa wajumbe wa bodi waliteuliwa ni Kissa Vivian Kilindu,Juma Mkobya, DK Haji Semboja, Shabaan Kayungilo, Dk Mtesigwa Maingu , Bodi Mhegi, Felix Kabodya pamoja na Nyamajeje Weggoro. Katika hatua nyingine Bodi hiyo imeanza kazi januari 1 na itaishia Februari 31 mwaka 2017.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: