Vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya maarufu Mteja wameitaka serikali na jamii kuwapa msaada wa kifikra na mawazo ili kuwajenga katika mtazamo hasi wa matumizi ya dawa hizo sambamba na kufanya jitihada za kuwakomboa katika matumizi ya dawa za kulevya.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa mtandao wa HIVI SASA vijana hao wamezitaja sababu zinazowapelekea kujikita na matumizi ya dawa hizo ni pamoja na kukosa shughuli maalumu za kufanya suala linalowapelekea kuwa na msukumo wa ushawishi kutoka kwa vijana wenzao unaowapelekea kutumia dawa hizo.
Aidha vijana hao wameeleza kuwa licha ya kujihusisha na matumizi ya dawa hizo wengi wao wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo maambukizi ya VVU na kifua kikuu (TB) kutokana na ulevi huo kuhusisha matumizi ya kuchangia bomba za sindano na hali ya usafi wa miili yao jambo linalosababisha ongezeko la magonjwa ya VVU na kifua kikuu (TB).
Katika hatua nyingi vijana hao wameyashauri makundi mbalimbali ya vijana yanayozidi kujitokeza kwa sasa kufanya mambo yatakayowajenga kimaisha na si kukimbilia katika matumizi ya dawa za kulevya ili kupunguza idadi za waathirika wa dawa hizo kwa lengo kuongeza nguvu kazi ya vijana kwa maslahi ya Taifa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment