Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, ameamua kuibeba Ndanda FC.
Ili kuhakikisha klabu ya Ndanda FC inafanya vizuri katika mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, ameamua kuishika mkono timu hiyo kwa kuisaidia kitita cha Tsh. Milioni 4.5.
Hawa Ghasia, ambaye pia ni Mbunge wa Mtwara vijijini, ametoa kiasi hicho ikiwa ni pamoja na posho za wachezaji kwa wiki, ili kuinusuru timu hiyo isishuke daraja na hivyo kuendelea kuwakirisha Mkoa wa Mtwara katika ligi kuu Tanzania bara.
Ndanda inashikilia mkia katika msimamo wa ligi kuu kufuatia kuwa na pointi sita ikiwa imeshinda michezo miwili na kupoteza michezo sita hivyo kujikuta katika wakati mgumu.
Msemaji wa Ndanda, Idrisa Bandari alifunguka kuwa kiasi hicho cha fedha kitasaidia timu hiyo kuwa katika kiwango kizuri ambapo waziri pia ameahidi kutoa posho ya shilingi milioni 1.2 kwa wiki hadi msimu utakapoisha.
Mbunge huyo alitoa kiasi hicho kutokana na kukabiliwa na ukata ambapo kiasi cha shilingi milioni 3 zitatumika kwa ajili ya malazi na chakula huku milioni 1.5 kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vya michezo kwa wachezaji.
Sawa fungu limetoka kwa Waziri huyo, lakini kwa mwenendo wa Ndanda katika ligi hii yenye upinzani mkubwa kwa sasa watabaki ligi kuu msimu ujao?
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment