Leo ni siku ya kukumbuku ya Kifo cha Dr Martin Luther King aliyefariki dunia tarehe 4 Aprili 1968 kwa kupigwa risasi ambapo leo anatimiza miaka 47 tangu afariki dunia.
Dr Martin Luther King,Junior alikuwa ni Mchungaji wa Kibaptisti na Mwanahakati mashuhuri kutoka nchi ya Marekani aliyepigania haki za binadamu. Dr Martin luther jr alizaliwa tarehe 15 Januari 1929 mjini Atlanta, Georgia, Marekani. Alikuwa ni mtoto wa mzee Martin Luther king Sr. Ambaye pia alikuwa ni kiongozi wa kupigania haki za binadamu. Mnamo mwaka 1964 alitunukiwa tuzo ya Nobel ya Amani.
Jina la Martin Luther King Jr. si geni masikioni mwa watu (wakiwemo wanaharakati vijana wa sasa, ukiacha kundi kubwa la wazee). Martin Luther King Jr. mwanaharakati na mpigania haki za binadamu, hususani wamarekani weusi.
Mwanaharakati huyu ambaye ameacha jina ambalo halitafutika katika historia ya kupigania haki hapa duniani alikuwa kiongozi maarufu wa changamoto za kuhakikisha ya kwamba weusi katika Marekani wanapata haki sawa na weupe.
King aliupinga waziwazi ubaguzi wa rangi, na alisisitiza umuhimu wa weusi kupatiwa elimu ya mpaka ngazi ya chuo kikuu bure. Mwaka 1955 King aliongoza mgomo huko Montgomery ambao ulikuwa unapinga unyanyasaji na ubaguzi katika mabasi, na mwaka 1963 aliongoza maandamano maarufu kama “Maandamano ya Washington” ambapo alitoa hotuba yake maarufu ya “Nina Ndoto” (I have a Dream).
Katika hotuba hiyo baadhi ya maneno yake yametumiwa hivi karibuni hata na Rais wa Marekani, Barack Obama wakati wa kampeni za kumuingiza jumba jeupe (State House). Mbali na kupata tuzo ya Nobel miaka minne kabla ya kifo chake (1964).
Kiongozi huyo alikuwa na mchango wa kupinga ubaguzi wa rangi na unyanyasaji kwa kutumia njia ya amani. King alianzisha na kuwa Rais wa kwanza wa Southern Christian Leadership Conference mwaka 1957. Mpaka kipindi cha kifo chake, King alijikita kupigia upatu jitihada za kumaliza umasikini na kupinga waziwazi vita vya Vietnam (akitumia mtazamo wa kidini pia).
King anaendelea kuenziwa pamoja na kwamba kimwili hayupo duniani, na miongoni mwa tuzo alizojipatia baada ya kifo chake ni Presidential Medal of Freedom (1977) pamoja na Congressional Gold Medal (2004).
Marekani iliitangaza Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari kila mwaka kuwa sikukuu ya kitaifa ya King kama ishara ya kumuenzi.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment