Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara, Azam FC, kesho Januari 20, Siku ya jumanne, wanatarajia kushuka dimba kutetea ubingwa wao wakiminyana na Kagera Sugar katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Azam FC wamekwishatua Mwanza tayari kwa mchezo huo, huku wakiwa na kumbukumbu ya ushindi mwembamba wa bao moja bila dhidi ya Stand United, mchezo uliopigwa juzi jumamosi katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, bao hilo pekee la Azam lilifungwa na Kiungo Frank Domayo katika dakika ya 43 baada ya kukaa nje ya Uwanja kwa muda mrefu akifanyiwa matibabu.
Kwa upande wa Kagera Sugar ambao ndio wenyeji wa mchezo, watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao moja bila kutoka Mbeya City ambao walikuwa katika nafasi ya pili kutoka mkiani mwa ligi wakiwa na pointi nane, licha ya Kagera kuwa katika nafasi ya tano wakiwa na pointi 14.
Mchezo huo wa kesho kati ya Azam FC na Kagera Sugar unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa sana na wakuvutia kutokana na timu zote kwa sasa kuhitaji matokeo ya Ushindi, Azam watakuwa wanataka pointi tatu ili kujiweka sehemu nzuri ya kutetea Ubingwa wao na Kagera wakitaka kuhakikisha wanamaliza ligi kuu wakiwa katika nafasi mbili za juu.
Kagera Sugar kwa sasa inatumia uwanja huo wa CCM Kirumba kama uwanja wa nyumbani kufatia Uwanja wake wa Kaitaba kuwa katika marekebisho ambapo FIFA wanauwekea Nyasi bandia.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment