PAC: Misamaha ya kodi yazidi kupaa Tanzania

Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) inadaiwa kusababisha misamaha ya kodi kuzidi kupaa nchini Tanzania. Hatua hiyo inafuatia Rais kuto saini sheria hiyo jambo linalopelekea kukithiri kwa misamaha hiyo nchini Tanzania. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati hiyo, Kabwe Zitto wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dares salaam jana kuhusu kauli ya Ikulu kushangazwa na kamati hiyo kuendelea kulalamikia misamaha ya kodi, wakati wameshindwa kupitisha muswada wa Sheria utakaosaidia kufuta misamaha ya kodi nchini. Mwenyekiti huyo amesema “Si kweli kwamba hatujapitisha sheria, Mkurugenzi wa Ikulu aangalie taarifa zake vizuri, Sheria hii tayari imepitishwa ila mpaka sasa haijatekelezwa na ndio maana madhara ya misamaha ya kodi inazidi kuendelea,” Ameongeza kuwa taarifa ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaonesha kuzidi kupanda kwa misamaha ya kodi ambayo imefikia kiasi cha Sh trilioni 1.82 kwa mwaka wa fedha 2013/ 2014. Zitto amemwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) awasiliane na Serikali ili kubaini chanzo na sababu zinazofanya sheria kutotangazwa kwenye gazeti la Serikali. Kamati hiyo imemuagiza Waziri wa Fedha kuitangaza Sheria hiyo kwenye gazeti la Serikali ili iweze kutekelezwa. Sheria hiyo ya VAT iliyotakiwa kutekelezwa tangu Januari mwaka huu, ina wigo mkubwa wa kupunguza tatizo la misamaha ya kodi endapo Serikal itaifanyia kazi mapema.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: