Wataalamu wa Afya wamezitaja faida zinazotokana na ulaji wa bamia ni kuongeza kinga dhidi ya magonjwa ya figo, saratani pamoja na pumu ikiwa ni pamoja na kutibu maradhi mbalimbali ya mfumo wa chakula ikiwemo vidonda vya tumbo na mengine yanayofanana kwa kupata hauweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia.
Wataalamu hao wameeleza kuwa endapo mtu atazingatia katika ulaji wa bamia ana uwezekano mkubwa wa wa kujiondoa katika hatari ya kupata maradhi hayo hata kuboresha uwezo wa macho kuona kutokana na bamia kubeba chanzo cha Vitamini A na Beta Carotene ambavyo ni virutubisho vinavyosaidia uwezo wa kuona.
Hata hivyo Bamia imetajwa kuwa ni moja ya chanzo kinachosaidia kuweka kawaida kiwango cha sukari mwilini na nyuzinyuzi zake zinasaidia kurahisisha ufyonzwaji wa sukari mwilini na kuacha mwili ukiwa katika sukari ya hali ya kawaida huku ikifanya mifupa kimarika zaidi.
Aidha Bamia imepewa sifa ya kudhibiti kiwango cha lehemu mwilini na hasa pale mtu anapotumia vyakula vingi vyenye mafuta ikiwa ni pamoja na kusaidia katika mmeng’enyo wa chakula kwa kulainisha choo.
Kwa kuzingatia haya jamii inashauriwa kula Bamia mara kwa mara kama kinga ya magonjwa yaliyotajwa hapo juu ikiwa ni pamoja na kuimarisha miili yao kukumbwa na matatizo mbalimbali.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment