WAZIRI JUMA NKAMIA ANUSURIKA KUPIGWA NA WANANCHI WA JIMBO LAKE
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Juma Nkamia amenusurika kupigwa na wananchi jimboni kwake baada ya kutoa kauli zenye kejeli.
Nkamia ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Kusini alikumbwa na hali hiyo wiki iliyopita alipokua katika kijiji cha Nchemba alipokwenda kuwanadi wagombea wa CCM katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika wiki iliyopita.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho alisema Nkamia aliponzwa na kauli za kejeli alizozitoa dhidi ya aliyekua Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Msongozli Yahaya kutoka CUF.
Mkamia alimtuhumu Mwenyekiti huyo kwamba amekua akimchafulia mbele ya wananchi wake kwa lengo la kumkwamisha katika uchaguzi ujao”Pamoja na kutoa maneno mengi ya kejeli hali ya hewa ilianza kuchafuka pale ambapo Nkamia alipoagiza wasaidizi wake wamkamate mwenyekiti huyo aliyekua amekaa pembeni na kumpeleka katika gari lake.
Baada ya hali hiyo wananachi walianza kuzunguka gari la Nkamia huku wakiwa na mawe ili kuhakikisha Mwenyekiti wao hakamatwi huku Nkamia akilizimika kuingia ndani ya gari na kuondoka kwa hofu ya kupigwa.
chanzo:gazeti la mtanzania
0 comments:
Post a Comment