UF:Waziri Mkuu na Waziri wa TAMISEMI wawajibishwe

Jivunie kuwa mwana ludewa


Chama cha Wananchi - CUF kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kumuwajibisha Waziri Mkuu na Waziri wa TAMISEMI kwa kushindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa baada ya kuibuka dosari kubwa zikiwemo kukosekana kwa wino, majina ya wananchi na karatasi za kupigia kura jambo lililoleta vurugu na kusababisha vituo vingi kurudiwa uchaguzi.
  
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba ametaka serikali kutekeleza makubaliano ya vyama vya siasa na TAMISEMI yaliyotaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo iwe na dhamana ya kusimamia uchaguzi, pamoja na daftari la wapiga kura litumike katika uchaguzi wa serikali za mita pamoja na kuingizwa kwa kipengele cha maadili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aidha kutokana na vurugu zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika baadhi ya maeneo, Profesa Lipumba amelitahadharisha jeshi la polisi kuacha kutumia nguvu kwa ajili ya kulinda maslahi ya baadhi ya vyama ili kuepusha vurugu zisizo za lazima katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: