Watu 2 wapigwa na kuvuliwa nguo nyumbani kwa Wema, ni mafundi wake waliodaiwa kuiba
Nyumbani kwa Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu, kumetokea tukio la kushangaza la watu wawili wanaodaiwa kuwa mafundi, kupigwa na kudhalilishwa kwa kuachwa uchi wakidaiwa kuhusika na wizi.
Akizungumza na Mpekuzi jana, jirani wa Wema aliyetambulika kwa jina la Mama Steve, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa majira ya saa 5 asubuhi mpaka saa 9 jioni.
“Waliopigwa na kulazwa chini uchi wa mnyama ni mafundi ambao wanakujaga kila siku kumtengenezea Wema nyumba yake,”amesema mama huyo.
“Sasa baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka, baada ya kuondoka wakaitwa tena na kuambiwa kuna simu imeibiwa ndani, ndo mtiti ukaanza.”
“Petit akatumwa akachukue mabaunsa 7 na baada ya kufika wakapandisha muziki mpaka mwisho ili sisi tusisikie nini kinaendelea huko ndani. Sasa kuna mtu alikuwa anapita hapa kwenye geti lao akasikia mtu analia sana ikambidi akachungulie ndo akamkuta fundi watu wawili wamelazwa chini uchi wa mnyama wanapigwa na hawana nguvu kabisa!
"Ndo yule jamaa kwakuwa alikuwa anamjua yule fundi akaita watu wakaanza kugonga geti ili wafungue lakini hawajafungua geti. Tukawa tunasikia sauti ya Wema ikisema ‘jamani waacheni hao mtawaua’ lakini anasema hivyo wakati yeye inaonyesha ndo alikuwa kinara wa matukio hayo.
"Wema ana roho ya kikatili sana. Amefanya matukio mengi lakini hivyo hapana! Yaani kama anataka usalama wake anatakiwa ahame vinginevyo vijana watamfanyika tukio la kinyama sana,”ameongeza mama huyo.
“Baada ya watu kuwa wengi sana pale nje ndo geti likafunguliwa watu wakaingia na kuwachukua wale vijana wakiwa hawajitambui na wapo uchi ndo wakapelekwa hospitali.
"Sasa baada ya kupelekwa hospitali polisi wa kituo cha Mabatini na wao wakagonga geti wakawa hawataki kulifungua polisi wakapindukia na kuingia ndo wakawakamata baadhi ya watu na kuondoka nao.
"Hilo ndo tukio alilolifanya mwanadada wenu ambaye anadai alikuwa Miss Tanzania,”alisema Mama Steve.
Pia shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Samira, alisema amesikitishwa na tukio hilo la kinyama.
“Hii ni tabia yake, hata wafanyakazi wake wa ndani anao kaa nao saa zingine anawapiga makofi! Kwakuwa ni ndani kwa ndani sisi majirani hatufuatilii, lakini kwa hilo na sauti yake tumeisikia japo watu wake wanadai hakuwepo,”alisema.
Baada ya taarifa hiyo, Mpekuzi ilimtafuta mjumbe wa nyumba kumi, Mwarami ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai hataki kuliongelea sana kwakuwa limeshafika katika kituo cha polisi Mabatini.
Pia Mpekuzi ilifika katika kituo cha polisi Mabatini ili kujua nini kinaendelea katika tuhuma hizo lakini iliambiwa kumuona mkuu wa kituo ambaye hata hivyo hakuwepo kwa muda huo.
Mtu wa karibu wa Wema, Petit Man aliyetajwa kuhusika kwenye tukio hilo, amesema kuwa watu hao walipigwa lakini hawakuvuliwa nguo.
“Yeah kuna tukio limetokwa,lakini hakuna mtu aliyevuliwa nguo,”alisema Petit na baada ya hapo alikata simu.
>>>>MPEKUZI
0 comments:
Post a Comment