MAANDALIZI YA SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA HAPO KESHO YAKAMILIKA
Maandaliziya siku ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) Desemba 9, kutimiza miaka 53, yanaendelea Uwanja wa Uhuru ambapo kutakuwa na gwaride la kijeshi vikundi vya sanaa, kwaya, halaiki ya vijana, ‘brass band’ na matarumbeta.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amesema milango katika Uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi ambapo wananchi watakaofika katika hafla hiyo watatumia mlango wa kusini upande wa Barabara ya Mandela kuingia uwanjani, na waalikwa wenye kadi watatumia mlango wa geti namba 2 na viongozi watatumia geti namba tatu 3.
0 comments:
Post a Comment