WANAUME WANAOFANYIWA UKATILI MKOANI RUVUMA WAANZA KUJITOKEZA

Matukio ya wanaume kunyanyaswa na kufanyiwa ukatili na wake zao ikiwemo kumwagiwa maji ya moto na hata wengine kukatwa viungo vyao yameshika kasi mkoani Ruvuma ambapo baadhi ya wanaume wameanza kuripoti matukio ya kunyanyaswa na wake zao katika madawati ya Jinsia. Hayo yameelezwa na wanaharakati wa haki za binadamu kwenye kongamano la maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia lililoandaliwa na shirika la kuhudumia watoto yatima Ruvuma (ROA) la Mkoani Ruvuma. Akifungua kongamano hilo mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Mkirikiti amewataka wanawake kuwafundisha mabinti kuheshimu ndoa zao ili kukomesha unyanyasaji huo
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: