VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAJUMUISHWA RASMI KATIKA VITA DHIDI YA UJANGIL

i wish u happy chrismass and ney year

Baadhi ya maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Tanapa na mradi wa Spanest wakati wakishiriki kikao cha siku moja cha kuimarisha mikakati yao inayolenga kukabili ujangili
Ndani ya darasa

MRADI wa Kuboresha Mtandao wa Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST) unazidi kuimarisha mikakati ya kuwalinda tembo na wanyama wengine dhidi ya vitendo vya ujangili.

Wakati ikiendelea kuimarisha mafunzo ya askari wa wanyamapori wa hifadhi zilizoko katika ukanda huo, ikichangia magari kwa ajili ya doria na ikiwa katika mpango wa kuwafunga viongozi wa tembo vifaa maalumu vya mawasiliano vya kuratibu mwenendo wa tembo hifadhini:

Juzi SPANEST inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) na serikali ya Tanzania imewakutanisha wajumbe wa kikosi kazi na wawakilishi kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakiwemo viongozi wa jeshi la Polisi, wanasheria, uhamiaji na usalama wa Taifa wa mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Dodoma na Singida.

Mratibu wa SPANEST, Godwell Ole Meing’ataki alisema lengo la kikao hicho kilichofanyika mjini Iringa ni kuwashirikisha wadau kutoka katika sekta ya ulinzi na usalama ili kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha ushiriki wa wadau katika usimamizi wa rasilimali na kukabiliana na ujangili.

“Suala la ujangili ni suala linalohitaji ushirikiano mkubwa, haliwezi kumalizwa na mamlaka moja, na hivi vyombo vya ulinzi na usalama ni muhimu sana katika mapambano haya  ya kukomesha ujangili,” alisema.

Akifungua mkutano huo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema ujangili ni tatizo kubwa katika nchi na bara la Afrika.

“waliokuwepo wakati tukipata Uhuru wanaweza kutoa ushahidi kwamba tulikuwa na tembo wengi sana, lakini wamepungua kwa kasi inayotishia mnyama huyo kutoweka kama mikakati ya kupambana na ujangili haitapata ushirikiano wa wadau wote,” alisema.

Mungi alisema ni lazima yawekwe mazingira yatakayowafanya watu waone wanaguswa kama wanavyoguswa pale wanapoibiwa mali zao.

“Ujangili ukiendelea kwa kasi namna hii unaleta mtazamo hasi kwa dola, unadhohofisha na kuzalilisha sheria za nchi na hivyo heshima ya nchi inapungua,” alisema.

Kwa upande wa vyombo vya dola, Mungi alisema heshima yake itaporomoka na kudhalilika kama jitihada zake hazitaonesha matunda mazuri katika kulisaidia taifa kukabiliana na ujangili.

“Dola yetu ikidhalilika kwasababu ya ujangili, sisi tunadhalilika zaidi. Tupitie mkakati wa kupambana na ujangili ili tujielekeze vizuri katika kupunguza ujangili,” alisema.

Alisema ndani ya mkakati kuna sera, kuna rasilimali na vitendo vya utendaji ambavyo kama vitatumika kwa pamoja ujangili ni lazima utakwisha.

Mbali na mada iliyohusua sekta ya wanyamapori na umuhimu wa uhifadhi, mada nyingine zilizotolewa katika kikao hicho ni pamoja na ya changamoto za upelelezi wa kesi za wanyamapori, ya changamoto ya uendeshaji wa kesi za wanyamapori na iliyohusu umuhimu wa ushirikiano katika ulinzi wa wanyamapori.

Pamoja na kuibua mpango kazi wa pamoja, kikao hicho kilimalizika kwa kuanzisha kikosi kazi cha kanda ya Ruaha Rungwa kitakachokuwa kikifuatilia mambo mbalimbali yanayohusu ulinzi wa wanyamapori katika ukanda huo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: