WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAKAZI, ANNA TIBAIJUKA AMETENGULIWA RASMI NAFASI YAKE YA UWAZIRI, PROF MUHONGO AWEKWA KIPORO

i wish u happy chrismass and ney year



Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akihutubia taifa la Tanzania kupitia wazee wa mkoa wa Dar es salaam jioni hii 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Anna Tibaijuka ametenguliwa rasmi nafasi yake ya Uwaziri na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete amesema wamemueleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka kuachia ngazi ili apate kuteua waziri mwingine.

Kuhusu Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Rais Kikwete amesema huyu amemuweka kiporo kwanza maana bado uchunguzi unafanyika.



"Waziri wa ardhi Tibaijuka kupokea pesa za Escrow , tumekaa nae na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa ajili gani na amesema ni za shule, mengi yameelezwa. Maswali makubwa kwa nini hazijaenda shuleni moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema ndo masharti ya mtoaji, tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa kimaadili kuhusu kupokea hizi pesa, tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue mwingine.

Waziri Muhongo huyu tumwemweka kiporo,
Waziri wa nishati na madini tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi nimeagiza ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya maadili pia wanafanya kwa ajili ya kupata maamuzi kwa misingi ya haki.
Nitafanya maamuzi siku hizi mbili tatu",Rais Kikwete

Rais Jakaya Kikwete ametengua nafasi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kupitia hotuba aliyotoa kuzungumzia kashfa ya upotevu wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
Hatua hiyo imechukuliwa na Rais Kikwete mbele ya wazee wa Dar Es Salaam aliokuwa akiongea nao na matangazo kurushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa na vyombo vingine.
Uchunguzi uliofanywa na kamati ya hesabu za umma ya Tanzania (PAC), ilidai kuwa Profesa Tibaijuka ni mmoja wa watu walionufaika kinyume cha sheria kwa kupata fedha zilizotoka katika akauti hiyo iliyofunguliwa kutunza fedha kusubiri ufumbuzi wa mgogoro wa kibiashara kati ya kampuni ya kusambaza umeme TANESCO na kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL.
Siku chache zilizopita Profesa Tibaijuja aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kubainisha kuwa hakuwa akikusudia kujiuzulu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Hata hivyo Rais Kikwete hakutangaza kuwachukulia hatua watumishi wengine waliodaiwa kuhusika na tuhuma hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi zaidi unatakiwa kwa kila mtuhumiwa.
Kumekuwa na ubishi mkubwa kujadili endapo fedha ambazo ni mabilioni zilizochukuliwa zilikuwa za umma au la. Na hata Rais Kikwete amesema maelezo aliyopewa na wataalam yanaonyesha hazikuwa mali ya TANESCO.



Prof. Anna Tibaijuka aliyeng'olewa uwaziri jioni hii nchini Tanzania.Unakumbuka wiki iliyopita Waziri Anna Tibaijuka alijitapa kuwa akijiuzulu hata Rais Kikwete atamshangaaa? Lakini cha ajabu leo Rais Kikwete amemtaka atoke kwenye nafasi hiyo ya Uwaziri na achaguliwe mtu mwingine.


Prof. Sospeter Muhongo aliyewekwa kiporo

Nimepita katika ukurasa wa Facebook wa Mwandishi wa habari Dotto Bulendu  yeye ametoa mchanganuo huu  juu ya hotuba ya Rais Kikwete

 
PESA ZA ESCROW SI ZA UMMA,ASEMA RAISI KIKWETE,
-ANADAI SERIKALI HAIKUPATA HASARA YOYOTE KUTOKANA NA SAKATA HILI,
-ATENGUA UTEUZI WA PROF TIBAIJUKA KWA KUKUBALI KUWEKEWA PESA KWENYE AKAUTI YAKE BINAFSI.
-AMUWEKA KIPORO PROF MUHONGO,WAKATI UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA,AKIPATA MAJIBU ATATOA UAMUZI.
-APANGUA BAADHI YA MAPENDEKEZO YA BUNGE.
-ADAI CCM WALIKUWA IMARA KWENYE SAKATA LA ESCROW
-AWATAKA CCM NAO WAKAWAAMBIE WANANCHI KUHUSU ESCROW
-AKIRI KUWA UJAMAA USHAKUFA KITAMBO
,huu ndi mchanganuo wa aliyoyasema raisikkikwete kuhusu ESCROW hii leo.
i) AMEKIRI KUWA TANESCO ILIKUWA INAIBIWA NA IPTL
ii) TRH 5.7.2006 NDIYO ACCOUNT YA TEGETA ILIFUNGULIWA NA KUFIKIA TAMATI TRH 5.9.2013 MAHAKAMA ILIAMURU SHUGHULI ZOTE ZA TANESCO ZIKABIDHIWE KWA IPTL HUKU KUKIWA HAKUNA KESI ILIYOFUNGULIWA ACHILIA MBALI ILE YA MWANZONI YA MALALAMIKO YA TANESCO KUWA WANAIBIWA KUPITIA CAPACITY CHARGE
iii). PESA ZILIKAA KWENYE ACCOUNT YA ESCROW KWA MIAKA 7.
iv) .Wakati CAG anakagua kulikuwa na shilingi 202 Bilioni nukta tisa.
v) Kama Tanesco wangeli tozo za uwekezaji,akaunti hii ingekuwa na shilingi Bilini 306.7,kutokana na Tanesco kutolipa ilibaki na madeniya shilingi Dola Bilioni 33.6 na IPTL.

vi) .Account ya Ecsrow haikuwa na Bilioni 306,bali zilikuwemo Bil 202 pekee ambazo IPTL ilikuwa inaidai Tanesco.
vii).Amesema kuwa kutoka na hali ya mgogoro ulivyokuwa pesa zilizokuwa ndani ya akaunti ya ESCROW SI ZA UMMA BALI NI ZA IPTL kwani ndiyo mlipwaji kutokana na madeni ambayo IPTL inaidai TANESCO kutokana na tozo za uwekezaji.

vii).Kuhusu majibu ya CAG,kuhusu pesa ni za nani?raisi amesema kama Tanesco wangeshinda mgogoro wao na IPTL basi pesa hizo zingekuwa za UMMA kama ilivyokuwa kwenye kesi yao ya mwaka 2001,ila kwa sababu Tanesco walishindwa,pesa hizi ni za IPTL na si UMMA(PUBLIC)

viii),KUHUSU KUWEMO KWA KODI ZA SERIKALI NDANI YA ESCROW ACCOUNT KIASI CHA BILIONI 21 NA MILIONI 700,AMESEMA PAP WALIPELEKEWA DENI LA KODI YA SERIKALI,AMESEMA CAG ALIKAGUA NA KUSEMA PESA ZILIZOKUWEMO KWENYE AKAUNTI YA ESCROW HAZIKUWA NA SIFA ZA KUITWA PESA ZA UMMA.

ix).Trh 15.9.2013 mahakama kuu ya Tanzania ulifanya uamuzi wa maombi ya kampuni ya VIP kuomba kusimamisha mchakato wa kuuza hiza za IPTL wakilumbana juu ya hisa,uamuzi wa mahakama ulikuwa PAP wapewe hisa 30 NA WAKANUNUA HISA 70 na waliandikisha hisa 70 Brela,mahakama ikaamua hisa zikabidhiwe PAP ambao ndiyo mmiliki halali wa IPTL.,Uamuzi huu wa mahakama ulimaanisha kuwa PAP wanatakiwa kumiliki mpaka pesa za ESCROW kwa PAP,umauzi ambao ulizuia malumbano serikalini juu ya akauniti ifungwe ama isifunwe,pesa zitoke ama zisitoke.

x).Wizara ya nishati na madini waliamu kuomba ushauri kwa mwanasheria mkuu juu ya pesa,AG alielekeza kuwa pesa zilipwe kama mahakama ilivyotaka,benki kuu waliuliza maswali haya,na AG akaelekeza walipe kwa PAP na hakuna kodi,ushsuri wa AG uliitoa nafasi ya akaunti kufungwa na kugawanywa rasmi na baadae kuingia barabarani.

xi).Maamuzi yote yaliyofanyika yalifanyika kwa maelekezo ya mwanasheria mkuu,umuzi huu wa mwansheria kuu umeibua mjadala mkuu kuwa kuna rushwa kubwa,watu wamemegewa mshiko,kila mtu kaongea.

xii).Amekanusha kuwa kufungwa kwa akaunti ya ESCROW hakukuwa na msukumo kutoka kwa maafisa wa serikali,amesema serikali ilifanya juhudi kubwa kwenye sakata hili.

xii).Amesema mwanasheria mkuu alimwambia hakukuwa na makosa yeyote kwenye maamuzi ya mahakama,na pia hakuna hasara ambayo serikali imepata kutokana na sakata hili la ECSROW kwa sababu pesa hizo zilikuwa ni deni ambalo Tanesco ilikuwa inadaiwa na IPTL.

xiii).Kuhusu kuwa PAP walinunua hisa za PIPAL LINK huku kikuwa na amri ya mahakama ya kutouza hisa,amesema bado vyombo vya mamlaka vinachunguza

xiv).Kuhusu uuzwaji wa hisa,amesema napo kunahitaji uchunguzi zaidi hasa bei ya hizi hisa.

xv).Amesema Rugemalira alilipa kodi aliyokuwa anadaiwa kiasi cha shilingi Bilioni 38,RUGEMALIRA hana makosa kwenye hili,Alilipa kodi zote.

xvi).KUHUSU MAPENDEKEZO CAG ameelekeza taaifa zile zipelekwe PCCB.

xvii).Kuhusu waliomegemewa pesa na RUGEMALIRA,amesema Takukuru na tume ya maadili ya watumishi wa umma wanachunguza na kushuhulika na watumishi wa umma wote waliopewa pesa,amesema tume ya maadili ya umma itawahoji wote waliopewa pesa.
KUHUSU MAZIMIO YA BUNGE

i.Amesema serikali imeyapokea maazimio na itayafanyia kazi

ii.Kuhusu kutaifisha mitambo ya IPTL,amesema si sawa kutaifisha sababu kutafukuza wawekezaji

iii.Kuhusu uwazi wa mikataba,amesema serikali itafanya mapitio ya mikataba,amesema kuna haja ya serikali na bunge kukaa pamoja na kuzungumza,kwa sababu kuna makampuni yanataka usiri wa mikataba(company secret)

iv)Kuhusu PCCB,na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vichukue hatua,amesema tayari utekelezaji ueanza.

v).Kuhusu kuwavua vyeo wenyevitio wa kamati amesema bunge ndilo litekeleza.

vi).Kuhusu kuundwa kwa tume ya kijaji kuwachunguza majaji waliohusika na sakata la ESCROW,amesema itabidi kuzingatia utaratibu wa kikatiba na sheria,amese suala hili linatakiwa kuanzia kwenye mahakama,halianzii kwa raisi wala bungeni,Amemuachia Jaji mkuu alishughulikie na kumpelekea mapendekezo raisi.

vii).Kuhusu mamlaka husika za kifedha na kiuchunguzi ziitaje Stanbic bank na benk zilizohusika zitangazwe kuwa taasisi zinazotakatisha fedha amesema uchunguzwe na mamlaka husika.

viii).Kuhusu serikali iandae na kuwasilisha marekebisho ya sheria ya uundwaji wa rushwa kubwa,amesema hilo ni wazo zuri,na serikaliimekuwa inaifanyia marekebisho taasisi ya kuzuia rushwa tangia mwaka 2008

ix).Kuhusu kuwavua nafasi zao watumishi wa umma wakiwemo mawaziri waliotajwa,raisi Kikwete amesema,Bodi ya Tanesco imeshamaliza muda wake,hili lishajifuta,kuhusu katibu mkuu Maswi amesema mamlaka zinazohusika zianze ushunguzi wa kuchunguza tuhuma zake,mwanasheria mkuu ameshajiuzulu,kuhusu mawaziri(TIBAIJUKA) amesema wamezungumza nae na wamekubaliana aachie ngazi,kuhusu Prof Muhongo amemuweka kiporo.


Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: