VIWANGO VIPYA VYA FIDIA KUPUNGUZA KERO AJALI NCHINI ?

Mkurugenzi Kanda ya Mashariki ( CHAKUA) Bw Thomas Haule. Chama cha kutetea Abiria nchini Tanzania kimeitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha viwango vipya vya fidia kwa wafu na majeruhi katika ajali mbalimbali nchini Tanzania. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dares salaam Mkurugenzi Kanda ya Mashariki ( CHAKUA) Bw Thomas Haule amesema kuwa iwapo serikali itaidhinisha viwango vipya vya fidia na kuvifanya viwe katika kanuni za fidia katika nchi itasaidia sana kupunguza ajali. Viwango vipya elekezi vya fidia ni kama ifuatavyo: (a) Kukatika mkono fidia yake iwe milioni 100 (b) Kuvunjika mkono fidia yake iwe milioni 50 (c) Kuvunjika mguu milioni milioni 50 (d) Kukatika mguu milioni 120 (e) Kuvunjika shingo milioni 100 (f) Kuvunjika kichwa na kuchanganyikiwa – mwenye familia milioni 200 – ambaye hana familia milioni 100 (g) Kupoteza kidole,meno,pua,sikio milioni 30 (h)Kupoteza jicho/ kuvunjika bega milioni 40 (i)Kufa na kuacha mke na watoto 2 milioni 150 Ameongeza kuwa viwango hivi vya fidia viwe kwenye bima, na endapo serikali itavikubali basi itasaidia wamiliki kuogopa na hivyo kuhakikisha kwamba ajali hizo hazitokei tena kwa kuajiri madereva wenye taaluma, kutoingiza magari mabovu pamoja na kuhakikisha madereva hawaendi mwendo kasi
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: