CHAKUA YATOA ONYO DHIDI YA UPANDISHAJI HOLELA NAULI MWISHO WA MWAKA

Chama cha kutetea Abiria nchini Tanzania (CHAKUA) kimewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri na wafanya kazi wao kuacha kabisa tabia ya kupandisha nauli nyakati za mwisho wa Mwaka pamoja na sikukuu mbalimbali suala ambalo ni kinyume na sheria zilizowekwa na Sumatra. Kwa mujibu wa Mkurugenzi ( CHAKUA) Kanda ya Mashariki Bw Thomas Haule maesema kwamba katika kipindi cha mwisho wa mwaka wamiliki wa mabasi ya pamoja na wafanyakazi wamekuwa na mazoea ya kupandisha nauli suala lililoota mizizi na kupelekea abaria kupata usumbufu mkubwa. Mtandao wa hivisasa umefika katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo Mikoani Ubungo ambapo umebaini kuwa bado kuna mabasi yaliyopandisha nauli ambapo abiria wanalipishwa pesa tofauti na iliyoandikwa kwenye tiketi. Kwa mfano nauli ya kutoka Dar es salaam kwenda Ruvuma ni elfu 40,000. Kwenye tiketi imeandikwa elfu 40,000 na lakini wapiga debe wanaiuza kwa bei zaidi ya hiyo. Katika hatua nyingine Chakua kimewataka abiria wote wanaosafiri kipindi cha mwisho wa mwaka kutoa taarifa kwenye mamlaka husika ikiwemo jeshi la Polisi usalama barabarani, Sumatra pamoja na Chama cha kutetea abiria Tanzania bila uoga ikiwa wanalipishwa tofauti na kiwango halisi cha bei kilichoandikwa kwenye tiketi
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: