TRL KUWATIMUA WATENDAJI WASIOKUWA NA TIJA

Serikali kupitia waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe imeibuka na kubainisha kuwa inatarajia kuwatangaza watendaji wasio kuwa na tija kwenye shirika la Reli Tanzania TRL wiki ijayo. Akizungumza na watendaji wa shirika hilo mkoani Mwanza Mwakyembe amesema serikali imejidhatiti kuwekeza katika shirika hilo ili tija ionekane na kama tija haionekani, uongozi wa juu una tatizo. Alisisitiza kuwa hatuwezi kunyima pesa sekta nyingine halafu reli ikabaki vile vile miaka nenda rudi na kuwataka wafanye kazi kwa ubunifu. Aliongeza kuwa katika kipindi kifupi serikali imenunua mabehewa 270 pamoja na kutoa fedha zingine kwa ajili ya kununua mabehewa 210 na vichwa 13 vimeagizwa. Kwa upande mwingine alisema shirika hilo lilianzishwa ili liweze kujitegemea, lakini limeshindwa kujitegemea na serikali inaendelea kulipa watumishi suala ambalo linakinzana na dhamira ya serikali ya kutaka shirika hilo lijitegemee
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: