MBEYA CITY DARAJA LA YANGA KUONGOZA LIGI WIKI HII?

Baada ya jana kuambulia pointi moja katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara, raundi ya nane dhidi ya Azam FC, katika uwanja wa Taifa, sasa Klabu ya Yanga inajipanga kukalia uskani wa ligi hiyo hapo mwisho mwa wiki hii itakapo wavaa Mbeya City. Huenda Yanga ikakaa kwenye kilele cha msimamo wa VPL hapo Januari 3 mwakani atakapokutana Mbeya City katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Jana Desemba 28 Yanga ilicheza na Azam FC katika uwanja wa Taifa jijiini Dar es salaam na kuambulia pointi moja baada ya kufungana 2-2, mabao ya Yanga yakifungwa na Amisi Tambwe, pamoja na Simon Msuva, huku kwa upande wa Azam FC wao walijipatia mabao hayo kupitia kwa Didier Kavumbagu na Nahodha John Bocco Adebayor. Mchezo kati ya Yanga na Mbeya City unatazamiwa kuwa, ndio utakao ipaisha Yanga hadi katika kilele cha ligi hiyo kufatia mwendo wa kusua sua walionao Mbeya City katika msimu huu, tofauti na mwaka jana ambapo hadi mzunguko wa kwanza wa ligi unamalizika ilikuwa haijafungwa mchezo wowote lakini kwa sasa ipo nafasi ya tatu kutoka mkiani ikiwa na pointi nane tu. Endapo Yanga itashinda katika mchezo huo dhidi ya Mbiya City, itawarazimu waombe dua mbaya kwa Mtibwa Sugar ambao wanaongoza ligi kwa pointi 16 ambapo watakutana na Azam wenye pointi 14 sawa na Yanga.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: