TIBAIJUKA KUTETEA JIMBO LA MULEBA 2015

Mbunge wa Jimbo la Muleba Prof. Anna Tibaijuka amesisitiza kuwa ataendelea kukitetea kiti chake cha Ubunge katika Jimbo la Muleba licha kutokea kashfa ya sakata la Ecrow lililopelekea kuvuliwa uwaziri. Akizungumza na wananchi katika jimbo la Muleba Tibaijuka amesema kuwa wananchi hawakumchagua yeye kama waziri bali walimchagua kama mwakilishi wao. Hata hivyo amewaonya wapinzani wake wa kisiasa hivi karibuni kwamba yeye ndiyo chaguo bora la wapiga kura wa jimbo la Muleba. Katika hatua nyingine Tibaijuka aling’olewa uwaziri na Rais Jakaya Kikwete kutokana na kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kupokea kiasi cha shilingi bilioni 1.6 fedha zilizokuwa na mgogoro kati ya kampuni ya uwekezaji ya IPTL na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: