ORODHA KAMILI YA WANAOWANIA TUZO ZA TASWA 2013/2014

KAMATI ya Kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam jana na kupitia majina ya wanamichezo waliopendekezwa kuwania tuzo hizo. Tuzo itafanyika Desemba 12 mwaka huu ukumbi wa Diamond, Jubilee (VIP), Dar es Salaam, ambapo wanamichezo mbalimbali waliofanya vizuri kati ya Juni 2013 hadi Juni 2014 watakabidhiwa tuzo zao. Ni imani yetu kwamba zaidi ya wanamichezo 40 watakabidhiwa tuzo zao siku hiyo, ambapo kamati imejiridhisha kwamba wanaowania tuzo hiyo wanastahili kulingana na mapendekezo ya vyama vya michezo kupitia Kamati zao za Ufundi. Mshindi wa kila tuzo ataingia katika mchakato wa kumpata Mwanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2013/2014, ambapo pia siku hiyo ya sherehe za tuzo itatangazwa zawadi ya Tuzo ya Heshima kwa yule ambaye itaonekana alikuwa na mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya kimichezo hapa nchini. Tuzo hizo ni kuanzia Juni 2013 hadi Juni 2014. OLIMPIKI MAALUM: Wanaume: Raphael Kalukula, Pazi Mwinyimkuu na Hatibu Matali wanawake: Blandina Blasi, Shida Jaha na Mwanaharusi Risasi. MPIRA WA KIKAPU; Wanaume:Lusajo Samwel (Oilers), Erick Mchemba (ABC) wanawake:Sajda Ahmed Lyamaiga(Don Bosco Lioness), Rehema Silomba (Don Bosco Lioness) na Orlyn Titus (Don Bosco Lioness). MPIRA WA MAGONGO; Wanaume:Yohana Wilson, Focus Paul, Deep Vaja Wanawake: Valentina Quarantta, Kidawa Seremala na Mary Mhina MPIRA WA WAVU: Wanawake:Yasinta Remmy (Jeshi Stars), Hellena Richard (Magereza) na Teddy Abwao (Jeshi Stars). WanaumE: Kelvin Peter Severino (Magereza), Nassoro Sharifu (Jeshi Stars) na Athuman Rupia (Jeshi Stars). RIADHA: Wanawake: Zakia Mrisho, Jaqueline Sakilu na Catherine Lange Wanaume:Alphonce Felix, Dickson Marwa na Fabian Nelson. BAISKELI: Wanawake: Salome Donald, Martha Anthon na Sophia Adson. Wanaume: Richard Laizer, Hamisi Mskala na Gerald Konda, GOFU: Wanaume:Nuru Mollel, Abasi Adam na Frank Mwinuka Wanawake: Madina Iddi, Hawa Wanyeche na Angel Eaton GOFU YA KULIPWA: Hassan Kadio, Yassin Salehe na Geoffrey Leverian JUDO Wanaume: KOMBO Masoud Amour, MBAROUK MbaroukSleiman Wanawake: Grace Alfonce Mhanga, Salma Omari Othman. TENISI WALEMAVU: Wanaume;Novatus Emmanuel Temba,Yohana Assa Mwila, Juma Mohamed Hamisi Wanawake; Rehema Selemani Saidi,Bihawa Mustafa Ituji TENISI: Wanaume: Tumaini Martin, Emmanuel Malya na Omari Sulle Wanawake: Rehema Athumani, Edna John, Georgina Kaindoh NETIBOLi: Doritha Mbunda (JKT Mbweni), Berina Kazinja (Magereza Moro), Andressa Andrea (Magereza Moro) Ngumi za Ridhaa: Fabian Gaudence, Ahmed Furahisha na Ally Abdul Ahmed SOKA; Wanawake: Sophia Mwasikili, Sherida Bonifacena Amina Ally WANAUME Elias Maguli (Ruvu Shooting-sasa Simba), Erasto Nyoni (Azam FC) na Nadir Haroub (Yanga). WACHEZAJI WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA Kipre Tchetche (Azam), Amis Tambwe (Simba) na Mbuyu Twite (Yanga). WATANZANIA WANAOCHEZA NJE Richard Laizer (baiskeli-Afrika Kusini/Uswisi) Mbwana Sammata (TP Mazembe-soka DRC), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe-soka DRC). NGUMI KULIPWA, Francis Cheka, Ramadhani Shauri na Said Mbelwa. MPIRA WA MIKONO Wanaume: Hemedi Salehe (JKT), Msafiri Makoti (Ngome) na Abinery Kusena (JKT) Wanawake: Veronica Mapunda, Subira Omary na Mwajabu Lugato WANAMICHEZO CHIPUKIZI Omari Sulle (tenisi) Sheridah Boniface (soka wanawake) Aishi Manula (soka wanaume-Azam) MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA 2013/2014: ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA KATEGORI. TUZO YA HESHIMA: Itatangazwa ukumbini siku ya sherehe Desemba 12 mwaka huu. Rehure Nyaulawa Mwenyekiti Kamati ya Tuzo 03/12/2014
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: