Matokeo ya mechi za Ligi kuu ya England
Ligi kuu ya England imeendelea usiku huu kwa michezo mine iliyozikutanisha timu nane za ligi hiyo .
Kwenye uwanja wa Emirates , Arsenal waliweza kushinda mchezo wao wa pili mfululizo baada ya kuwafunga Southampton 1-0 ukiwa ni ushindi wao wa pili mfululizo wakishinda kwa bao moja .
Bao hilo lililowapa Arsenal ushindi lilifungwa na Alexis Sanchez ukiwa ushindi wa kwanza kwa Arsenal dhidi ya timu iliyoko kwenye nafasi za tatu bora .
Alexis Sanchez ameifungia Arsenal mabao 8 kwenye EPL msimu huu.
Kwingineko Chelsea walishinda mchezo wao dhidi ya Tottenham kwa matokeo ya 3-0 . Ushindi huo ulikuja baada ya mabao ya Edin Hazard , Didier Drogba na Loic Remy .
Edin Hazard akifunga bao la kwanza kwa chelsea.
Mshambuliaji Didier Drogba akifunga bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Tottenham.
Katika mchezo mwingine Hull City na Everton walitoka sare ya 1-1 , na Man city wakawafunga Sunderland 1-4 .
Matokeo haya yanamaanisha kuwa Chelsea wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 33 wakiwa wamewazidi Man city kwa pointi sita , Southampton ambao leo hii wamepoteza mchezo wao wa pili mfululizo wamejikuta wakishuka zaidi huku tofauti yao na Man United inayoshika nafasi ya 4 ikiwa pointi moja pekee .
0 comments:
Post a Comment