ONE DAY YES sehemu ya 5

Jivunie kuwa mwana ludewa
ONE DAY YES


Sehemu Ya 5

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana ↓

"Au unafatiliza ule msemo unaosemwa kua kila goti litapigwa mbele za bwana??"
"mi sijui bwana we sema"
"haya sasa nisemeje sasa?"


"SEMA HIVI,.... eee mizimu yetu na ya mke wangu pamoja na yote. leo nipo hapa kusema ukweli kua kama nimemsaliti mke wangu naomba mniadhibu kwa kunikata uume wangu na kuniotesha manynyoo....SEMA HIVYO TU"
"heeeeeeeeeee ivi kweli mke wangu unanitakia heri kweli wewe? yaani niote manyoyoo aseeee?"

ENDELEAA



Daaa nilikua kama nafanya utani lakini mke wangu alikua siriasi kweli tena alikua hacheki kabisa wala kutabasamu. nikajua hapa kweli mke wangu kakasirika. afu sipendi nimkasirishe kwa jambo ambalo halina maana...
"lakini mke wangu si uliniambia mwenyewe jamani?"
"sasa mbona ulikua unaniambia uongo?"
Mke wangu aliondoka pale kwa hasira nami nikamfata mpaka pale alipo na kuanza kumbembeleza. Kiukweli ni kweli aliniambia mwenyewe kua nichepuke ili nisimuumize mtoto wetu. ila alinipa nafasi hiii tu
"naomba usije ukarudia tena"
"sirudii haki ya mungu vile sirudii tena"
Basi swala lile liliisha kiivyo huku tukikumbatiana kwa mapenzi moto moto.
"mmhhh hebu niambie mimi na huyo nani anakatika kiuno vizuri?"
"mmhhh aiseee humkuti yule binti ni noma kwa mauno"
"nini?? pumbavu ndio maana sijataka uende..."
Mke wangu alikua ananipiga kwa vibao huku tukikimbizana kiutani
"basi nilikudanganya... ni wewe ndio unakatika vizuri"
Basi ilikua ni moja ya utani wa hapa na pale kwa mimi na mke wangu tu..

Baada ya siku hio kupita na sasa ni Jioni mida ya saa 10 hivi nikiwa nipo zangu kitaa nikiendelea kuaga aga marafiki, ndugu, na jamaa ili nilalie safiri kesho.. Nilipokua kitaani mara nilimuona sabrina akishushwa na school bus kutoka shuleni.
Sikutaka kumshtua wala kumshobokea kitu. Bali nilikauka kama sio mimi vile Lakini haikuseidia kitu kwani hata kushuka kule sii kua ndio kituo chake bali alishuka kwasababu kaniona mimi.
"chidi? chidi? jamani si nakuita?"
"ooo sory nilikua nipo na mawazo sana mambo vp lakini?"
"poa tu.. sasa mtoto mdogo hivyo una mawazo gani?"
"si ile pesa ulionipa jana niliidondosha muda sio mrefu na ni maeneo haya haya tu"
Nilimdanganya kua imepotea ile elfu 50 ili kama anayo nyingine anipe
"pole chidi ila usijali. we twende mjini sasa hivi"
"mjini? mjini kufanyaje?"
"we twende tu chidi"
Tukisema mjini hatumaanishi labda ni sehemu ya kusafiri kwa umbali hapana... ni sawa na dare slam kwa mtu aliopo dar vijijini afu akitaka kwenda kariakoo ni lazima aseme niende mjini... maana huko anapoishi ni vijijini japo ni dar hio hio...
Sasa sisi tulikua tanga vijijini huko maeneo ya pangani katika kijiji kiitwacho KIKOKWE hivyo amesema twende tanga mjini...
Basi nami sikukataa tulipanda gari flani linalokwenda huko... tena ni kwa nauli yake mwenyewe. Nilikua sina wasi wasi...

Ilituchukua masaa machache hadi kufika tanga mjini.. kisha tukawa tunaelekea katika maduka flan hivi ya simu... nikajua hapa lazma ninunuliwe simu.
Tulipofika pale mtoto aliongea na yule muudumu wa duka kua anahitaji tecno moja nzuri ya batani... afu akanigeukia mimi na kuniambia
"chidi usijali kwani nakununulia simu mpyaa... tena ya maana"
"mmhh nitashukuru lakini si ghali sana mamii?"
"wala tu usjali. kwani baadhi ya maduka ya simu hapa tanga ni yakwetu"
"haaaaaa acha utani sabrina"
"kweli chidi tuna maduka yasiopungua 7 hapa stend"
"mmhhhh kumbe mpo vizuri eee?"
"mmm wala tu kawaida bwanaa.. ila chidi si tutafanya vile vitu vyetu?"
"mmhhh lini?"
"mi nataka na leo bwana"
"aaahhh bwana tufanye kesho"
"aaa mi staki bwana chidi"
"kweli sabrina tufanye kesho au jioni kwenye mdumange pale"
"kweli chidi utakuja?"
"nitakuja kweli"
Basi tuliahidiana kiivyo huku nikiwa na furaha kwa kununuliwa simu ambayo maisha yangu yote nisingeweza kuinunua hio simu. japo haikua tachi skrini lakini alinunuliwa kwa gharama ya shiling elfu 60 keshi...
Nilipewa ile simu huku nikicheka cheka kimtindo, Tulimaliza kununua simu kisha tukaingia hotelini tukapiga msosi wa maana ambao sijawahi kula msosi uliojaa kuku na rosti ya maana.... kwani mwisho wangu wa kula nyama ya bata ni kipindi mke wangu alipojifungua tena nilikula mamiguu na vichwa tuu na shingo..vingine alikula mke wangu sasa leo nimetengewa vyuku mezani na nyama choma bila kusahau chips mayai... afu ni kila mtu na msahani wake Kiukweli mimi sio mlaji sana wa vitu vya mafuta hivyo niligusa tu kidogo na kumkumbuka mke wangu...
Nilimuita weita aniletee mfuko kisha nikaviweka kwenye mfuko, Sabrina alishangaa kuona kituko kama hicho. Baada ya kuona vile akaniuliza kua
"heeeee mbona unakiweka umo?"
"daaa vtu vya mafuta hua vinanishibishaga haraka sjui kwanini"
"jamani pole sasa hivyo unapeleka wapi?"
"nina mdogo wangu nyumbani wacha akale kuliko tutupe"
Nilimdanganya kua nina mdogo wangu lakini sio kweli... ila nimemkumbuka tu mke wangu....maana sabrina hajui kama nina mke. na akijua heeee hata hii simu huenda nikanyang'anywa muda si mrefu
"apana bwana mchukulie vingine... weitaa lete teka wei ya kuku na chips mayani pamoja na nusu nyama choma"
"haaaaaa sabrina nina ndugu mmoja tu zote hizo za nini?"
"nimefrai kwakua unajali ndugu zako"
Basi mavitu yalikusanywa na kuwekwa kwenye rambo moja na ile yangu pia niliiweka huko huko ila hajaona... mana anataka kile chakula changu nilichobakiza nikitupe, na wakati hakijaliwa kabisa yani niligusa gusa tuu kwa kua nimemkumbuka mke wangu na mtoto wangu....
Baada ya hapo zikaletwa na mango juice kama 6 hivi... tukajazia rambo kisha akalipa shiling elfu 40 khaaaaa pesa ndefu ile mbaya. yaani hivi vimsosi tu bili imekuja elfu 40???? duuuuuu kweli mjini pesa

Basi tulitoka pale muda ya saa 12 jioni tukapanda gari ya kurudi kikokwe tulipotoka... Muda huo kagiza kaliingia kiasi flani hivyo huko ndani ya gari tulikua tukidendeka vibaya mno
"chidi?"
"sema?"
"plz nakuomba usikose kuja ngomani"
"usijali nitakuja"
Basi ilikua tupo katika hali ya kutamaniana kimtindo lakini tulijizuia kidogo...

Tulifika kikokwe mida ya saa 2 usiku huku mtoto akaita toyo impeleke kwao na mimi pia akanilipia toyo inipeleke kwangu afu akanikatia kitu kama elfu 30 hivi
Kisha kila mtu akasepetuka zake kwao..

Nilipofika nyumbani nilimkuta mama watoto kavimba ile mbaya hivyo niliutua mzigo wangu wa misosi ya maana. huku mke wangu akishangaa tu. Nilifungua mfuko wa mapocho pocho na kumkabidhi mke wangu ajisosomole... Nilichukua nyama kidogo na juice kisha nikampelekea mama angu pamoja na bibi.. Afu nikampa mama ile elfu 30 yote niliopewa na sabrina... Kisha nikamuaga mama angu kua kesho ndio naondoka..... Daaaa mama angu alinipa baraka nyingi sana huko niendako... na bibi pia nikamkatia ya ugoro na kunipa nae baraka nyingi sana.... binafsi nilifurahi sana kwa kuruhusiwa safari ya kwenda arusha.....

Niliporudi geto nilichukua chips moja na nyama rost ya kutosha na juice 2 ili nimpelekee broo juma na mke wake..... Baada ya hapo nilirudi na kuanza kusosomola na mke wangu...
"kabla sijala hiki chakula hebu niambie umekitoa wapi?"
"aaaaa mke wanguuuu maswali gani hayo unaniuliza?"
"we si useme tu"
"ok wacha nikuambie ukweli... nilikutana na sabrina mchana na akanipeleka mjini kuona maduka yao na hata simu hii hapa kaninunulia.. ndio tukanunua kila mtu chakula chake cha nyumbani kwao... ila hiki kanilipia yeye huyo sabrina"
"na nanii mumefanya?"
"wala tu... ila mke wangu? mi leo naomba nikuombe kitu leo"
"ah ah kwakua nimejua chakula kimetoka wapi tule kwanza afu uniombe hicho kitu baadae"
Basi nilimsikiliza mke wangu na kuanza kusosomola msosi ule uliobakia kwa ajili yetu.... msosi mwingi tuliugawa huko nje
"mmhhh kitamu ee?"
"eeee ndio uniachie sasa nichepuke chepuke"
"weeee mjinga nini wewe?? na sasa hivi unifanye hata kwa kondomu sikubali tena uende kwa huyo sabrina wako"
"aaaaaa wacha nikakilipie chakula cha watu kwa leo tu"
"sitaki nishasema sitakiiiiiiiiiii Aaaa"
"heeeeeeee sasa nitakilipaje?"
"kwaio we umepokea ili ukakilipie sio?"
"amna bana utani tuuuu"

Basi tulimaliza kula pale kisha tukaingia kulala, sasa mtoto wa kiume nilikua naomba alale ili nimtoroke niende kwenye mdumange. Nilikua namuangalia mke wangu kama kalala fofofo
"mke wangu? mke wangu? we mama saidi?"
"nini wewe?"
"mhhh Mbona hulali?"
"we wataka nilale ili iweje?"
"aaah amna we lala tuuu"
"Aaannhaaa kuumbeee sasa silali leo"
"ok poa wacha nikuambie ukweli.... mama saidi naomba niende dumange basi"
"nakuambia huko huendi ng'ooo"
"aaaaaa mosieeee niache niende"

HAHAHAHA UNAONA HICHO KISAMBAA HAPO JUU??? ETI MOSIEEE... DUUUU KWELI NAJUA JUA ASEEE

"hakuna cha mosie wala mgosi hapa yani huendi...kama wataka twende wote"
"aaahh sasa na mtoto utachezaje?"
"tunamuacha ndani"
"haaaaaaaaaaaaa basi siendi aisee"
"acha na tulale"
Daaahhh safari ya kwenda dumangeni ilishia hapo. basi tukawa tumelala zetu tu mida ya saa 3 hivi usiku...
"chidi mi nina hamu bwana tufanyeje?"
"aaa mi siwezi kumuaribu mtoto"
"kachukue kondom basi"
"sitaki je kondom ikipasuka je?"
"utavaa mbili au tatu"
"haaaaaaaaaaaa zote hizo nitapizi saa ngapi?"
"bwanaaaa baba saidi fanya hivyo"
Sasa nikaona yeeeeees huu huu ndio muda wa kwenda mdumange.
"sawa basi ngoja nikachukue"
"nakupa dakika tano tu urudi hapa"
"sawaaaa"

Nilipotoka tu nje nikampigia sabrina simu
"haloo sabrina upo wapi?"
"bado nipo nyumbani... navizia mlinzi alale niruke geti"
"mmhhh mi mwenyewe huku sipati muda"
"basi tufanye kesho"
"poa kesho basi"
Ilikua pia ni poa ila safari ya mdumange haijaisha maana nina muda mrefu sijaendaga mdumange nilienda kununua kondom kisha nikaziweka mfukoni... Sasa nikawa naelekea mdumange kuyakata mauno........ sasa kufika njiani niliona mtu kwenye mti kavaa nguo nyeupeee pyeeeeee... Nikajua labda huende ni kademu kalikua kananisubiri nini ili twende nae mdumange
Ikabidi niulize huku nikijiamini maana nikiangalia kiunoni yupo kama kafunga kibwebwe vile.. ila alikua kavaa nguo nyeupe mithili ya kanzu au gauni........
"wewe ni nani? Ulikua unaenda mdumange nini? Eti dada kwani unaitwa nani?"
Nilikua nina maswali mengi sana muda huo
Sasa nilipoona hanijibu niliendelea zangu na safari huku nikiwa kama mtu mwenye haraka....mida hio ilikua ni mida ya saa 4 usiku afu kumetuliaaaaaaaa naskia mdumange kwa mbali....
Sasa nilipofika mbele nikamkuta mwingine akiwa kavaa vile vile kama huyu huku nyuma yangu...
"Aaaahhh kumbe mpo wengi wengi? twendeni basi ili tuwahi"
Sasa kitu kilichonishtua ni pale nilipoona mtu wa tatu akiwa katika mavazi yale yale... ila staili aliokuja nayo sikuweza kuifahamu japo alikua kwa mbali kidogo.... kwani alikuja kwa kutokea chini ya aridhi.. sasa nimekuja kujua kumbe hawa sio watu kama nilivyotarajia.... maana watu wa tanga wanapokwenda kwenye vigodoro au mdumange hua wana tabia ya kuvaa madira (magauni ya kushonesha) yanayofanana.... sasa nikajua nao hawa ndio walewale wamama wa vigodoro..... kumbe sio watu waskini ya mungu.. sasa nimekumbuka shuka na wakati kumekucha...... sijakaa vizuri mara mwingine kaja na staili ile ile ya kutokea Aridhini.... ila huyu alikua kavaa gauni jeusiiiiiiii tiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: