MBUNGE WA JIMBO LA LUDEWA CCM MKOANI NJOMBE MH, DEO FILIKUNJOMBE AHAIDI KUKARABATI JENGO LA SHULE YA MSINGI LUDEWA MJINI

Akiwasilisha ahadi hizo desember 6 mwaka huu katika kikao kilichoitishwa kwa dharula na mbunge huyo katibu wakebw, Stanley Gowelealizitaja ahadi hizo kuwa atatoa bati 150 na mifuko ya saruji ambayo itatosha kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo ikiwa ni pamoja na kukubali ombi la kuwa mlezi wa shule hiyo pekee wilayani hapo. Hata hivyobw, gowelealiwataka wananchi wilayani hapa kuunga mkono jitihada za kimaendeleo zinazofanywa namh, mbungekwa kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kukamilisha ukarabati wa madarasa hayo kwa wakati ili kuwatengenezea wanafunzi wa shule hiyo mazingira bora ya kujisomea. Pamoja na hayo katika nyakati tofauti wananchi na viongozi mbalimbali waliohudhuria kikao hicho wamepongeza jitihada zinazofanywa na mbunge huyo katika kupigania maslahi ya taifa na kutoa mfano jinsi mbunge huyo alivyoweza kupigania pesa za akaunti ya tegeta ESCRO mara alipokuwa bungeni pamoja na kusimamia maendeleo ya wilaya yake. Aidha wananchi hao wamesema kuwa watahakikisha wanashirikiana kwa ukaribu na mbunge Filikunjombe katika kuleta mabadiliko katika wilaya ya ludewa katika mkoa wa njombe na kuongeza kuwa mbunge wao nimpiganaji wa haki za wananchi wa tanzania hivyo nilazima taifa la tanzania likubali kumtumia kiongozi huyo kwa kila jambo lenye manufaa kwa wananchi wa tanzania.Mwishoooo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: