LUDEWA WATAKIWA KUJIAJIRI ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA UMASKINI

Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani njombe bw, Juma Solomoni Madaha amewataka wananchi wilayani humo kujiunga katika vikundi vidogovidogo vinavyo jishughulisha na utoaji mikopo kwa wananchi ili kuweza kujikwamua na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wengi wilayani humo. Alitoa ushauri huo kwa wananchi hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi juu ya wananchi hao kujiajiri wao wenyewe kwakutumia fursa walizo nazo ili kujinufaisha kiuchumi pamoja na kuendesha maisha yao hasa familia zao ikiwa nipamoja na kuwasomesha watoto wao katika shule mbalimbali za msingi na sekondari kwa lengo la kuwajengea msingi wa maisha watoto wao. Aliyesimama ni mkuu wa wilaya ya ludewa mkoani njombe bw, JummaSolomoni Madaha akizungumza na wananchi Alisema kuna baadhi ya wanawake wamekuwa wakiwategemea sana waumezao katika mambo mbalimbali ya maisha hasa katika suala la kupata pesa ili kuweza kuendesha maisha ndani ya nyumba kitendo ambacho si sahihi kwakuwa hata wanawake wanauwezo wa kujiunga katika vikundi iliwaweze kupata mikopo kwaajili ya matumizi yao majumbani. Aliongeza kuwa kwasasa wanaume wengi wamekuwa wakijishughulisha na shughuli mbalimbali ili kuhakikisha familia zao zinaishi katika maisha mazuri hivyo ni jukumu la kila mwanamke wilayani ludewa kushirikiana na waumezao katika malezi ya familia zao majumbani. Hatahivyo alisema kuna vijana hawapendi kujishughulisha ili waweze kujipatia kipato badala yake wamekuwa wakiilaumu serikali kwakilajambo na kubaki bila kazi yeyote hivyo vijana hao hujiingiza katika makundi mabaya na kufanya vitendo vya uovu ambavyo vinahatarisha maisha yao. '' kuna baadhi ya vijana wao kazi yao ni kuilaumu serikali kuwa haiwasaidii kwa lolote na kubaki wamekaa bila kazi mwisho vijana hao huamua kujiingiza katika vikundi ambavyo havina maana kwao hivyo nawasii vijana hao wajiunge katika vikundi hivyo na kama wakishindwa basi wajiajiri wao katika kazi mbalimbali kwaajili ya kujipatia kipato chao cha kilasiku'' Mkuu huyo wa wilaya alitumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi wilayani ludewa kujihadhari na ugonjwa wa ukimwi kwakuwa mkoa wa njombe umekuwa ukiongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa asilimia 14.8 kwa nchi nzima ya tanzania .
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: